Matunda na faida zake mwilini description
Kitabu hiki kinakwenda kukletea faida za kula matunda mbalimbali. Ijulikane kuwa matunda ni katika vyakula ambavyo husaidia miili yetu kuongeza uwezo wake wa kujilinda dhidi ya maradhi. Kupitia matunda tunaweza kupata vitamini mbalimbali na madini pia.
Kitabu hiki kitakupa mwangaza na ufahamu juu ya aina tofauti tofauti za matunda na nini faida zake kwenye miili yetu. Pia utajifunza hasara ambazo unaweza kuzipata endapo hutakula baadhi ya matunda.