4.4
345 review
668.27 KB
Everyone
Content rating
159.2K
Downloads
Kinga ya Muislamu screenshot 1 Kinga ya Muislamu screenshot 2 Kinga ya Muislamu screenshot 3 Kinga ya Muislamu screenshot 4 Kinga ya Muislamu screenshot 5 Kinga ya Muislamu screenshot 6 Kinga ya Muislamu screenshot 7

About this product

Kinga ya Muislamu. Dua na Adhkaar.

Rating and review

4.4
345 ratings
5
4
3
2
1

Kinga ya Muislamu description


بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم

Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema (Duniani) Mwenye Kurehemu (Akhera)

UTANGULIZI
Hakika sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunamuomba Atuhifadhi na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Mwenyezi Mungu hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa wa kumuongoza. Nakiri kwamba, hapana apasaye kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke Yake, hana mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mtume Wake. Mwenyezi Mungu Amrehemu na Awarehemu jamaa zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.
Baada ya yaliyotangulia huu ni ufupi (Mukhtasar) wa kitabu kiitwacho “HISWN AL-MUSLIM MIN ADHKAAR AL-KITAAB WA SUNNAH”
Ninamuomba Mwenyezi Mungu kwa majina Yake mazuri, na sifa Zake zilizo juu, Ajaaliye kazi hii kuwa, imesafika lengo lake, kwa kutaka radhi zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukitawanya, hakika Yeye Mwenyezi Mungu Ndiye Muweza.
Mwenyezi Mungu Amrehemu Mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وسلم na Aali zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.
↓ Read more